mtwara regional referral hospital
(ligula RRH)

Kijue kichaa cha Mbwa

KIJUE KICHAA CHA MBWA

Na;- SHIRA S.MANGUBE
IDARA YA AFYA – KINGA
RRH – LIGULA


MALENGO YA MADA:

  • Kujua kichaa cha mbwa
  •  Jinsi ugonjwa unavyoenea
  • Muda wa dalili kujitokeza (Incubation period)
  • Kufahamu dalili zake kwa mtu
  • Makundi 3 ya aina ya jeraha
  • Kujua jinsi ya  kuhudumia mtu aliyetafunwa na mbwa mwenye kichaa
  • Kujua  tiba kinga inayopaswa kutolewa kwa mtu aliyeumwa na mbwa anayehisiwa kuwa na kichaa
  • Kujua mbinu zinazotumika kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa 

UGOJWA WA KICHAA CHA MBWA NI NINI?

Ugonjwa hatari  unaoenea toka kwa wanyama kwenda kwa binadamu (zoonotic disease) 

 husababishwa na virusi  aina ya RNA kundi la Lyssavirus, familia ya Rhabdoviridae. 

Kifo ni 100% kama mtu aliyeumwa na mbwa hatapatiwa tiba kinga


JINSI UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA UNAVYOENEA

KWA TANZANIA  MBWA NDIYE MWENEZAJI MKUU WA UGONJWA HUU KWA BINADAMU NA  KWA WANYAMA WENGINE KAMA NG’OMBE NK

JINSI UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA UNAVYOENEA

KATIKA MATUKIO MACHACHE KICHAA CHA MBWA HUWEZA KUENEA KWA:

  1. Njia ya hewa (Aerosolized virus)
  2.  Kwa njia ya kupandikizwa kiungo cha mwili (Transplantation of tissue) kama figo toka kwa mtu mwenye maambukizi ya ugojwa wa kichaa cha mbwa 

(TANZANIA HAIJAWAHI KUTOLEWA TAARIFA)

MUDA WA DALILI  KUJITOKEZA(INCUBATION PERIOD)

Siku 10 mpaka mwaka mmoja( Wastani ni  mwezi 1 hadi 2.

Hii hutegemeana na:

  1. Idadi ya virusi vilivyoingizwa mwilini
  2. Ukubwa wa eneo la mwili lililotafunwa
  3. Kinga binafsi ya mtu mwilini
  4. Aina ya kirusi kilichoingizwa mwilini
  5. Umbali  wa jereha kutoka kwenye mfumo wa fahamu

DALILI ZA UGONJWA WA KICHA CHA MBWA

UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA HUJITOKEZA  KWA NAMNA MBILI ZIFUATAZO:

  1. Kupooza mwili (Paralytic rabies)

       2.Kichaa moto (Furious rabies)

 

      Hatua zote hizi mbili hutanguliwa na  dalili zifuatazo:

  • Homa,kuumwa kichwa,mwili kuchoka,
  •  kichefuchefu,kutapika, kuwashwa sehemu mtu  alipoumwa na mbwa
  • kuwashwa na koo na kuwa 
  • kikohozi kisichotoa makohozi baada ya tukio la kutafunwa na mbwa  


      KICHAA BARIDI( PARALYITC RABIES)

       DALILI ZAKE:

  • Kuuma kwa misuli ya mwili
  • Kupumua kwa tabu
  • Kupooza kwa misuli ya mwili hususani miguu na mikono 
  • Kifo


       KICHAA MOTO(FURIOUS RABIES)

       DALILI ZAKE:

  • Kukakamaa misuli
  • Kushituka shituka
  • Kuhema kwa tabu
  • Kuogopa maji, upepo na mwangaza
  • Kuchanganyikiwa au kurukwa akili
  • Kifo

      NAMNA  3 ZA MTU KUPATA MAAMBUKIZI YA KICHAA CHA  MBWA (TYPE OF CONTACT EXPOSURE)

  • Kuguswa au kulabwa kwenye ngozi isiyokuwa na michubuko (Touching or feeding of animals/licks on intact skin)
  • Jeraha lisilotoa damu (Minor scratches or abrasions without bleeding)
  • Jeraha linalotoa damu (single or multiple transdermal bites


       HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEUMWA NA MBWA

  •  Osha  jeraha  kwa maji mengi yanayotiririka na sabuni
  •  Osha kwa maziwa au kimiminika chochote kama maji hayapatikani
  •  Safisha jeraha kutumia  antiseptic (k.m. dettol, spirit n.k)
  •  Wahi kituo cha Afya kupewa TT na tiba kinga(chanjo) ya kichaa cha mbwa


      TIBA KINGA (CHANJO) YA KICHAA CHA MBWA

  • Hutolewa kwa njia kuu mbili (2)
  • Njia ya misuli (Intra-muscular, IM)
  • Njia ya ngozi(intra-dermal, ID

      Njia ya ngozi(ID) inapendekezwa itumike badala ya njia ya misuli(IM) kwa sababu:

  • Humpunguzia mwathirika muda  wa kuhudhuria kituo cha tiba kupata chanjo
  • Gharama yake ni ndogo (chupa 1 vs 5)
  • Humjengea mtu kinga ndani ya siku (7) saba


       UTOAJI WA KINGA(CHANJO) YA KICHAA CHA MBWA KWA BINADAMU

      Njia ya misuli(IM) haipendekezwi kwa sababu zifuatazo

  • Ni  njia ya gharama sana
  • Mteja hupaswa kuhudhuria kituo cha tiba  mara tano
  • Humjengea mtu kinga baada ya siku 14


      UTARATIBU WA UTOAJI WA CHANJO YA KICHAA CHA MBWA

  • NJIA YA MISULI(IM) 1mlx5=5vials   SIKU 0, 3, 7, 14 na 28
  • NJIA YA NGOZI(ID) 0.2mlx4=0.8ml  SIKU  0, 3 , 7 na 28


      NB: Serum(RIG) hutolewa siku 0(40IU per Kg body-weight kwa  jeraha linalotoa damu tu.

  •  Mtu aliyepata chanjo mwaka mmoja nyuma na akaumwa tena na mbwa, apewe     SIKU 0  na 3

      KINGA KWA MTU ALIYEUMWA NA MBWA ANAYEHISIWA KUWA NA KICHAA

  • JERAHA LA MTU ALIYEUMWA NA MBWA ANAYEHISIWA KUWA NA KICHAA HALISHONWI, kama kushona ni lazima ifanyike baada ya muathirika kupatiwa serum(RIG)
  • Muathirika apatiwe Antibiotic na sindano ya Pepopunda (T.T) kumkinga na  pepopunda na magonjwa nyemelezi

    CHANJO KWA MAKUNDI MAALAMU
  • Wataalamu wa mifugo wanaoshiriki kampeni ya uchanjaji wa mbwa
  • Waokotaji wa mizoga ya mbwa waliogongwa na magari
  • Wataalamu wa maabara wanaofanya uchunguzi wa wanyama wanaohisiwa kuwa na kichaa  SIKU 0, 7 na siku ya 21 au 28


      MBINU ZA KUDHIBITI KICHAA CHA MBWA

  • Kuchanja mbwa na paka kila mwaka kwa zaidi ya asilimia 70 katika kila eneo lenye mbwa/paka
  • Kudhibiti idadi ya mbwa  kwenye kaya kulingana na uwezo wa kuwahudumia
  • Kudhibiti  mbwa wazururaji


     UFUATILIAJI WA UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA/ KUNG’ATWA NA MBWA

  • Ufuatiliaji wa wagojwa  waliong’atwa na mbwa anaesadikiwa kuwa na kicha hutolewa taarifa kila wiki & mwezi kwa mfumo wa IDSR (IDWE, Monthly) Ngazi ya Wizara ya Afya, Maendereo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto