mtwara regional referral hospital
(ligula RRH)

ijue homa ya ini na chanjo

CHANJO YA HOMA YA INI

Utangulizi,

Homa ya ini ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya aina mbalimbali. Virusi ambavyo vina athari kubwa kwenye mazingira yetu ni aina ya Hepatitis B, mbali ya aina C nayo kuweza kusababisha lakini kwa mara chache sana

Unavyoambukizwa.

Homa ya ini (hepatitis B) inambukizwa kwa njia zinazoshabihiana sana na ugonjwa wa UKIMWI kama vile kujamiana (ngono isiyo salama), kuwekewa damu ya mtu mwene virusi vya homa ya ini, kuchomwa na vitu vyenye ncha kali kama vile sindando zisizosalama, majimaji yatokayo mwilini, na  mate (kula denda la mtu aliyeambukizwa).

Matibabu ya ugonjwa.

Hadi sasa magonjwa mengi yanayosababishwa na Virusi hayana tiba maalum, matibabu ni kwa madhara tu mgonjwa anayoyapata, hivyo njia sahihi ya kuepukana na magonjwa haya mara nyingi huwa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi na kuchanjwa.

Chanjo ya homa ya ini (hepatitis B)

Hii ni chanjo yenye uwezo wa kukinga maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis B).  Chanjo hii hutolewa kwa dozi tatu kwa kipimo cha mili moja  (1 mls) kila dozi.

Dozi ya kwanza ni wakati wowote.

Dozi ya pili ni baada ya wiki nne (mwezi mmoja)

Dozi ya tatu ni baada ya miezi 6

Usalama wa chanjo

Chanjo hii ni salama baada ya kudhitishwa na shirika la Afya ulimwenguni (WHO) na mamlaka  mbalimbali za udhibiti wa dawa Nchini

Maudhi madogomadogo

Chanjo hii kama zilivyo chanjo nyingine unapopatiwa  (chomwa) kuna maumivu kidogo sehemu unayochomwa yanayoisha kwa muda mfupi sana na haina madhara yeyote.

Matunzo ya chanjo

Chanjo hii kama ilivyo chanjo zingine ni lazima itunzwe kwenye joto ridi 0C ( 2+ hadi 8+) yaani kwenye ubaridi toka zinakotengenezwa  hadi kwa mchanjwaji.