mtwara regional referral hospital
(ligula RRH)

Shinikizo kubwa la damu

 • Tumia kiasi kidogo sana cha chumvi wakati wa kupika
 •  Tumia viungo kama vitunguu saumu na tangawizi katika kuongeza ladha ya chakula badala ya kutumia chumvi kupita kiasi. Pendelea kutafuna tembe moja ya kitunguu saumu asubuhi na nyingine jioni kwa kila siku.         
 • Epuka unywaji wa vinwaji vyenye kola, kahawa, majani ya chai.
 • Pendelea kutumia mchanganyiko wa mdalasini, tangawizi na hiliki badala ya majani ya chai.
 • Epuka sukari na vyakula vyenye sukari nyingi kama soda, pipi, biskuti, keki, na asali.
 • Epuka kukaa muda mrefu bila kula
 • Tumia  nafaka zisizokobolewa
 • Pendelea vyakula jamii ya kunde kama maharage, kunde, choroko, mbaazi, njegere nk. Punguza ulaji wa nyama nyekundu
 • Kula mboga za majani kwa wingi katika kila mlo (mboga za majani zipikwe kwa kiasi kidogo cha mafuta kwani  zikiliwa chukuchuku virutubishi havitaweza kupatikana mwilini ipasavyo
 • Kula tunda saizi ya kati katika kila mlo (kiasi cha tunda ni sawa na ngumi moja). Pendelea kula tunda na maganda yake bila kumenya kama inawezekana mfano apple na embe ila zingatia usafi wa chakula, kwa machungwa ondoa ganda la nje na mbegu na kula na makapi yake yote yaliyobakia.  (pendelea kula tunda kuliko juisi ya matunda).
 • Pendelea kunywa maziwa yaliyopunguzwa mafuta (low fat) kwa maziwa ya mtindi na maziwa ya fresh ila usizidishe robo lita kwa siku (isizidi mililita 250).
 • Epuka kutumia mafuta mengi wakati wa kupika na iwapo  unatumia dawa, zingatia maelekezo  ya dawa uliyopewa na daktari.
 • Epuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara na fanya mazoezi.