mtwara regional referral hospital
(ligula RRH)

mgonjwa wa kisukari

Mambo ya msingi ya kuzingatia kwa mgonjwa wa kisukari

 • Epuka sukari na vyakula vyenye sukari nyingi kama soda, pipi, biskuti, keki, na asali.
 • Epuka kukaa muda mrefu bila kula kwani sukari itashuka
 • Tumia  nafaka zisizokobolewa
 • Tumia  vyakula jamii ya kunde kama maharage, kunde, choroko, mbaazi, njegere nk. Punguza ulaji wa nyama hususani nyama nyekundu
 • Kula mboga za majani kwa wingi angalau mikono miwili iliyojaa (mboga za majani zipikwe kwa kiasi kidogo cha mafuta kwani  zikiliwa chukuchuku virutubishi havitaweza kupatikana mwilini ipasavyo na pia epuka kutumia mafuta ya wanyama ), mbogamboga kama matango, pilipili hoho, kabichi, nyanya, nyanya chungu, biringanya  yafaa zitumike kiasi cha kutosha.  
 • Kula tunda saizi ya kati katika kila mlo (kiasi cha tunda ni sawa na ngumi moja). Pendelea kula tunda na maganda yake bila kumenya kama inawezekana mfano apple na embe ila zingatia usafi wa chakula, kwa machungwa ondoa ganda la nje na mbegu na kula na makapi  yote yaliyobakia.  (pendelea kula tunda kuliko juisi ya matunda).
 • Pendelea kunywa maziwa yaliyopunguzwa mafuta (low fat) kwa maziwa ya mtindi na maziwa ya fresh ila usizidishe robo lita kwa siku (isizidi mililita 250).
 • Epuka kutumia mafuta mengi wakati wa kupika
 • Tumia kiasi kidogo sana cha chumvi wakati wa kupika
 • Epuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara.
 • Epuka msongo wa mawazo. Fanya mazoezi ya mwili  dakika 30 au zaidi na kutokwa jasho angalau kwa siku mara moja.
 • Iwapo unatumia dawa, zingatia maelekezo ya dawa  uliyopewa na daktari.

Wasiliana na wataalamu wa Afya ili ujue uzito unaotakiwa kuwa nao.